Kemikali
za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu
dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic
Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu
kupata kensa. Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika
miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa,
kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA
baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa
binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli mwilini au kufanya mutation, kitendo
ambacho huweza kusababisha kensa. Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho
hufanyika kwa haraka sana kama vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa
sindano. Habari hii ni tahadhari kwa watu