Katika hali ambayo muda mrefu imekuwa ikifahamika kwamba dawa za folic acid
zinazotakiwa kuliwa na mama wajawazito zina faida kemkem kwa watoto wanozaliwa,
wataalamu hivi karibuni wameendelea kufahamu umuhimu wake zaidi. Siku zote kina
mama wajawazito wamekuwa wakishauriwa kula folic acid miezi mitatu kabla ya
kushika mimba, na pia kwa miezi kadhaa wakati wa ujauzito. Utafiti wa hivi
karibuni umeonyesha kwamba watoto ambao mama zao walikula folic acid kabla na
wakati wa ujauzito kwa kiasi kikubwa huwa hawachelewi kuzungumza. Uchunguzi huo
uliofanywa huko Norway kwa kuwashirikisha wanawake 40,000 umebainisha kwamba
wale ambao hawakula folic acid kabla na wakati walipokuwa na mimba wana
uwezekano mara dufu wa kuzaa watoto wenye matatizo ya kuchelewa kuongea kuliko
waliokula. Kwa mujibu wa utafiti huo uliochapisha kwenye Jarida la Marekani la
Taasisis ya Tiba (JAMA) kula folic acidi wiki 4 kabla ya ujauzito na kuendelea
hadi wiki 8 baada ya kutungwa mimba husaidia kupunguza hatari ya watoto
kushindwa kuongea hata wanapofikia miaka mitatu. Ingawa wataalamu wamekiri
hawajui ni namna gani folic acid inazuia watoto kuchelewa kuongea lakini
wanasema, kuna uwezekano dawa hizo zikawa zinataathira katika mfumo wa neva na
kuzuia tatizo hilo lisitokee.
Folic acid ni miongoni mwa tembe zinazohusiwa sana mama wajawazito kula, kwani inajulikana kuwa zinazuia watoto wachanga kuzaliwa wakiwa na ugonjwa unaoitwa 'neural tube defects' ambao ni matatizo katika sehemu ya chini ya ute wa mgongo ambapo mtoto mchanga huzaliwa huku ubongo wake ukiwa haukukua kabisa. Lakini ingawa hayo yote yanajuliakana shaka yangu ni kuwa je, mama wajawazito katika nchi zetu wanajua hilo au je, wanaelimusha juu ya umuhimu wa kula folic acid? Nadhani ni jukumu langu mie na wewe kuielimisha jamii.