VITUNGUU MAJI NI KINGA YA MAGONJWA YATOKANAYO NA BACTERIA
Kitunguu ni aina ya mboga ya jamii ya yungiyungi . Ni mboga yenye harufu kali
inayochangamsha na kinatakiwa kutumika
kikiwa kibichi mara baada ya kukikata.
Imethibitishwa kisayansi kuwa juice yake huuwa vijidudu vya
kinamasi na vya kifua kikuu, vijidudu hufa mara tu baada ya kunusa moshi wake.
Imethibitishwa kuwa kwenye kitunguu kuna viuaji sumu vyenye
nguvu zaidi ya penisilin(penicillin)na pia ndani yake inapatikana vitamin C,Kutokana na utafiti huo umeonyesha
kuwa tukitumia vitunguu vibichi mbali na kuongeza kinga za mwili pia hutibu
maradhi yote yatokanayo na bakteria na
pia huimarisha misuli ya mwili mara unavuta moshi wake.
Baadhi ya maradhi yaliyodhibitishwa kikinga na kutibiwa na
vitunguu ni pamoja na:-
- uvimbe wa mapafu(pneumonia)
- kukojoa kwa kupata maumivu,
-Pumu n.k
Kwa ukweli huo tunashauriwa kujenga tabia ya kutumia vitunguu vibichi hata ikiwezekana kila siku.
tujitahidi kwani ni mboga ambayo inapakitikana kwa urahisi na tunaitumia kila
siku katika vyakula vyetu ingawaje mara nyingi tunavichanganya katika mboga kwa
kuvipika,sasa tujitahidi kuwa tunavitumia vikiwa vibichi katika milo yetu ili
tuweze kujenga kinga za miili yetu na
kuwa wenye nguvu na afya njema;