WELCOME TO MHF, WE OFFER HEALTH SERVICES ON COMMUNITY EDUCATION ON PREVENTION AND CONTROL MEASURES OF DISEASES.

Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene

Sijui ni kwa nini unauliza dawa za kunenepa badala ya kuuliza njia zinazoweza kukufanya unenepe,kumbuka madawa yana side effects zake zinazoweza kuwa hatari pia kwa afya yako mfano kama unavyoona dawa za uzazi wa mpango.

Pia ni vema ukajua athari za unene kabla hujaanza kutumia siyo tu kwamba umbo lako litabadilika kabisa tofauti na ulivyo na unavyo tegemea mfano unataka unenepe kiasi ukajikuta umenenepeana nyama zinaning`inia tu lakini ujue unaanza kunyemelewa na magonjwa kama pressure nk.

Hata hivyo kuchagua kuwa mnene au mwembamba ni uamuzi wako binafsi,ila ningekushauri utumie njia za kawaida kuongeza unene kuliko madawa.Hata hivyo hatujui wembamba huo ni wa kuzaliwa nao,au unatokana na maradhi mwilini,au msongo wa mawazo.....ukishajua chanzo ni mwanzo wa kumaliza tatizo.

Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene

1.Kula chakula cha kutosha kila unapokula halafu chenye mafuta mengi,chakula chenye wanga zaidi nk.
2.Usikae muda mrefu bila kula chakula,muda kabla ya mlo mwingine usizidi masaa 4 au 3 halafu ukipata msosi kandamiza sawasawa.
3.Achana na mazoezi hasa yale ya kukimbia.
4.Kula chakula kingi kabla ya kwenda kulala.
5.Punguza mawazo
6.Punguza kula mboga za majani na matunda badala yake kandamiza nyama,maharage nk.
Kutimia njia za kawaida ni bora kwa sababu ukiona uzito umezidi unaachana na njia hizi lakini unene wa dawa wakati mwingine hata kama ukiacha kutumia zinakuwa zimeathiri mfumo wa asili wa utendaji kazi wa mwili huenda ukashindwa kuzuia tena